
+255 22 2926263
We are open 8 am - 5pm
TANZANIA ASSOCIATION OF OIL MARKETING COMPANIES
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Chama cha Wauzaji Mafuta kwa Jumla cha Tanzania (TAOMAC) kinafahamu hatua mbalimbali ambazo Serikali inachukua katika kuhakikisha bei za mafuta hazipandi nchini. TAOMAC inapenda kumpongeza Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa hatua hizi madhubutu anazochukua na pia inapenda kumhakikishia Mhe Rais na Waziri wa Nishati ushirikiano wetu wa juu kabisa katika kutafutia ufumbuzi changamoto zinazoikabiri sekta ndogo ya mafuta nchini ili kuhakikisha ufanisi na gharama nafuu kwa masilahi ya wadau wote.
Ongezeko la bei za mafuta katika vituo vya mafuta hivi karibuni limechangiwa kwa kiasi kikubwa na ongozeko la bei ya mafuta ghafi katika soko la dunia. Mnamo Juni 2020, bei za mafuta kwenye vituo vya mafuta nchini zilishuka kwa kuvunja rekodi kutokana na madhara ya kiuchumi yaliyosababishwa na UVIKO-19. Baada ya nchi nyingi kuanza kuruhu shughuli za kiuchumi kuendelea baada ya janga la UVIKO-19 kupungua, bei za mafuta ghafi duniani zimekuwa zikipanda mfululizo tangu Aprili 2020. Hii imechangia ongezeko la bei katika vituo vya mafuta nchini. Serikali na Makampuni ya Kuuza Mafuta hayahusiki na upandaji wa bei za mafuta. Grafu Na. 1 inaonyesha namna bei za mafuta ghafi katika soko la duniani yalivyopanda na Grafu Na. 2 inaonyesha ongezeko la bei za mafuta katika vituo vya mafuta nchini, ambapo inaonyesha wazi kuwa upo uhusiano, isipokuwa kuanzia Mwezi Septemba 2021 ambapo Serikali iliingilia kati katika mfumo kwenye upangaji wa bei
Mpaka sasa, upandaji wa bei za mafuta umethibitiwa na Serikali baada ya kuingilia mfumo wa upangaji wa bei mnamo 2 Septemba 2021 ambapo Serikali ilisitisha matumizi ya Bei Elekezi za Septemba 2021, ambazo zilichapishwa na EWURA siku ya 1 Septemba 2021 na Makampuni ya Kuuza mafuta waliambiwa waendelee kutumia Bei Elekezi za Mwezi Agosti 2021.
Mwezi Oktoba, 2021 Serikali ilichukua hatua Madhubuti za kupunguza baadha ya tozo kwenye mafuta ambazo zinalipwa kwenye taasisi mbalimbali za Serikali ili kupunguza bei za mafuta nchini. Hii imesaidia kidogo kuzuia ongezeko la bei kwenye vituo vya mafuta kwa Mwezi Oktoba 2021. Kwenye Grafu Na. 2, kuanzia Agosti mpaka Okoba, 2021 mstari wa grafu umelala, hii inaonyesha matokeo ya Serikali kuingilia mfumo wa upangaji bei kuanzia 2 Septemba 2021 na kuendelea.
Pamoja na kuwa hatua hizi zimesaidia bei kupungua, lakini zimekuwa na adhari mbaya kwa Makapuni ya Kuuza mafuta. Pamoja na hayo, Makampuni ya Kuuza Mafuta yameendelea kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kuendelea kuagiza mafuta na kuyasambaza nchini.
Grafu 1. Bei za Mafuta Ghafi Jan 2021-Nov 2021 (USD/Barrel)
Grafu 2: Bei za Rejareja (TZS/Ltr) za Petroli (DSM) Jan-Nov 2021
Kwa bahati mbaya, bei za mafuta zinaweza kuendelea kupanda kwa sababu bei za mafuta ghafi katika soko la dunia bado zinapanda. Kwa mfano, Goldman Sachs inabashiri kuwa bei za mafuta ghafi ziapanda mpaka $90 kwa pipa kufikia Disemba 2021 na $110 kwa pipa kufikia mwaka 2022. OPEC + wanatabiri kuwa bei za mafuta ghafi kwenye soko la dunia zitaendelea kupanda mpaka 2022. Hivyo, ni muhimu kwa umma wa Watanzania ukafahamu hizi taarifa.
Imetolewa na :
BODI YA WAKURUGENZI
1 Novemba 2021,
Dar es Salaam
POSTPONEMENT OF TAOMAC GALA DINNER
On behalf of the TAOMAC Board of Governance, We wish...
The Government has removed petroleum fee amounting to TShs100 per...
Crude oil prices rises to $100 per barrel, highest in 8 years
The future is gloomy as the crude oil prices hits...
The Government of Tanzania has appointed Baker Botts as its transaction advisor
The Government has appointed a U.S.-based law firm as its...
TANZANIA ASSOCIATION OF OIL MARKETING COMPANIES
TAARIFA KWA VYOMBO...